Journalism

  

LALA PEMA WALIBORA

Machozi yanatutoka, hatwachi katu kulia

Mioyo yasononeka, habari metufikia

Hakika twasikitika, waswahili tunalia

Lala walalapo wema, Profesa Walibora


Mauti yametufika, hivi kama tunaota

Mlima ukaanguka, simanzi ikatupata

Nyoyo zetu zateseka, hili sisi kutupata

Lala walalapo wema, Profesa Walibora


Sio peke Afrika, kotekote duniani

Kilio kinasikika, hata kule marekani

Jemedari metutoka, tufanye yapi yakini

Lala walalapo wema, Profesa Walibora


Tasnia meyumbika, na nyororo kulegea

Weye mkuu kutoka, kileleni kozoea

Walibora pumzika, ila tulikuzoea

Lala walalapo wema , Profesa Walibora


Aliyapenda Rabuka,muumba na Muumbua

Mapema akakutaka, kwake upige hatua

Hivi kwetu metutoka, ila kwake mekimbia

Lala walalapo wema, Profesa Walibora


Ken tutakukumbuka, amali metuachia

Siku njema hijafika, na dagaa metwozea

Mbona haraka hakika, mkono kutupungia?

Lala walalapo wema, Profesa Walibora


Peponi kapumzika, kwa Mola twakuombea

Kamsifu msifika, wewe aliyekutwaa

Na hutasahaulika, lugha livyopigania

Lala walalapo wema , Profesa Walibora


Bwana Were Idara ya Kiswahili

IFIKIE WAZAZI

# IFIKIE WAZAZI# Understanding the balance between friends and parents

As children become teenagers, they begin to spend more of their time alone …

read more

SPOKEN WORD

Beyond My Expectation It wasn’t what I expected it to be,

A walk in the park I thought it would be,

I thought it would be like one of the …

read more