Idara Ya Kiswahili

  

IDARA YA KISWAHILI

Idara ya Kiswahili inashughulikia somo la  Kiswahili ambalo ni la lazima katika shule za msingi na za upili.Katika  shule hii ya wasichana ya State house, walimu na wanafunzi hujikakamua vilivyo ili kuhakikisha kwamba ufanisi umepatikana.

Tangu kuanzishwa kwa mfumo wa elimu ya 8-4-4 , hakuna mwanafunzi aliyewahi kupata gredi ya E katika somo la Kiswahili.Mwaka wa 2015, matokeo ya Kiswahili yalikuwa 8.5 (Gredi B)

 

Shughuli za idara

a)     Kuwafunza wanafunzi Kiswahili.

b)    Kuwaandaa wanaunzi kwa mtihani wa kitaifa wa KCSE.

c)     Kuwaandaa wanafunzi ili kushiriki katika mashindano na tamasha za muziki na maigizo.

d)    Kuwashirikisha wanafunzi  katika mijadala shuleni na kwingineko kama shule zingine,katika redio na runinga .

e)     Kuwaelekeza wanafunzi katika  utunzi  wa kazi za Kiswahili kama mashairi, tamthilia na nyimbo.

f)      Kuwahamasisha wanafunzi kuhusu matumizi ya lugha sanifu na kupambana na kilugha cha sheng’.

 

WALIMU KATIKA IDARA YA KISWAHILI

Idara hii ina waalimu wakakamavu na wanaojikakamua kweli nao ni;

a)     Bi. Mungara -Mkuu wa Idara

b)    Bi. Mvati- mwaklimu wa Kiswahili na mkuu wa idara ya ushauri na maelekezi.

c)     Bi. Barasa -Msaidizi wa Mkuu wa Idara

d)    Bi. Kinuthia -Mwalimu wa Kiswahili

e)     Bi. Nabukhwesi - Mwalimu wa Kiswahili

f)      Bi. Mboya- Mwalimu wa Kiswahili

g)     Bwana Indindi – Mwalimu wa Kiswahili.

 

CHAMA CHA KISWAHILI

Idara ina chama cha Kiswahili kinachoongozwa na Bi. Barasa .Wao hushiriki katika majadiliano  na sanaa za Kiswahili.Wanafunzi husajiliwa wanapoingia kidato cha kwanza.

 

MALENGO

  • Kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi shuleni anaongea lugha sanifu.
  • Kuinua gredi ya somo la Kiswahili hadi gredi ya A.

CHANGAMOTO

  • Mawasiliano kwa lugha ya sheng’ miongoni mwa wanafunzi.
  • Imani potovu kuwa Kiswahili ni lugha ngumu .
  • Wanafunzi hawadwusu Kiswahili kama wafanyavyo masomo mengine hasa sayansi.

 

Ripoti na Bi Mungara

Mkuu wa Idara.

 

Journalism

LALA PEMA WALIBORA Machozi yanatutoka, hatwachi katu kulia

Mioyo yasononeka, habari metufikia

Hakika twasikitika, waswahili tunalia

Lala …

read more

IFIKIE WAZAZI

# IFIKIE WAZAZI# Understanding the balance between friends and parents

As children become teenagers, they begin to spend more of their time alone …

read more